DED MSANGA ASISITIZA NIDHAMU KWENYE MASHINDANO YA UMITASHUMTA NGAZI YA MKOA.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Bi. Happiness Msanga amewasisitiza Wanafunzi waliochaguliwa kuiwakilisha Wilaya ya Karagwe kwenye Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) kuendeleza nidhamu walioonyesha kipindi chote cha maandalizi ya mashindano hayo.
Bi.Happiness ametoa wito huo leo tarehe 25/05/2025 kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Kambarage wakati akiagana na Wanafunzi wanaokwenda kwenye Mashindano hayo yatakayofanyika Wilaya ya Muleba kuanzia kesho Mei 26 hadi 29, 2025.
" Mmekua na nidhamu kipindi chote cha maandalizi niwasihi muindeleze hata huko mnapokwenda kushindana kwasababu nidhamu ni moja ya silaha kubwa ya ushindi ambao ndio tunaoutarajia kutoka kwenu nendeni mkaitangaze Karagwe kwa mambo mema na nidhamu ya hali ya juu" Alisema Bi.Happiness.
Aidha, Bi. Happiness ametumia nafasi hiyo kuwataka Wanafunzi kutoa taarifa kwa Walimu na Walezi watakaokuwa nao kwenye mashindano endapo wanapokumbana na changamoto yeyote hasa kuhusiana na mambo ya ukatili wa kijinsia.
Mashindano ya UMITASHUMTA Kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoa wa Iringa kuanzia tarehe Juni 07, 2025 hadi Juni 18,2025 yakiwa na kauli mbiu isemayo " Viongozi Bora ni Msingi wa Maendeleo ya Taaluma, Sanaa na Michezo. Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na Utulivu".
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.