• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
KARAGWE DISTRICT COUNCIL
KARAGWE DISTRICT COUNCIL

United Republic of Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA KARAGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na dira
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu
        • Sekondari
        • Msingi
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Mazingira na Taka ngumu
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Ufugaji na Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Maji
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Inayokuja
    • Iliyotekelezwa
    • Inayoendelea
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Taarifa
    • Sheria
    • Mpango mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha

Huduma za Kielimu

  

SEKTA YA ELIMU

ELIMU YA MSINGI.
    Mwaka 2015  Wilaya ina jumla ya Shule za Msingi 117 zikiwemo za    serikali 110, zisizo za serikali 7. 

 

UANDIKISHAJI  WA DARASA LA KWANZA.
    Mwaka 2015  Wilaya imeweza kuandikisha jumla ya wanafunzi 6,663 (asilimia 92), wavulana  3,366 na wasichana 3,297 kati ya wanafunzi 7,246   waliotarajiwa kuandikishwa.
            
  IDADI  YA WANAFUNZI.
    Hadi  kufikia Juni mwaka 2016, Wilaya ya Karagwe ina jumla ya wanafunzi  61,223, wavulana 29,865 na wasichana 21,358 na  kwa shule zisizo za serikali zina wanafunzi wavulana 636  na wasichana 611, jumla 1,247. Kwa ujumla wa  shule za serikali na zisizo za serikali zina wavulana 30,501 na wasichana  31,969, jumla kuu 62,470.

 IDADI  YA WALIMU.
    Wilaya ina jumla ya walimu 1,396 wa  kike 601 na wa kiume 795. Hii ni  sawa  na uwiano wa 1:44 yaani mwalimu 1 kwa wanafunzi 44.  Hata  hivyo   bado upo upungufu wa walimu 379 hii ni  kutokana na wingi wa wanafunzi  wanaosajiliwa kuingia darasa la kwanza na  baadhi ya      walimu kustaafu.

MIUNDO  MBINU.
    Hali ya miundo mbinu katika Shule za  Msingi ni kama inavyoonyeshwa kwenye  jedwali hapo chini.

          Jedwali Namba 3  (Miundo mbinu ya shule za msingi kwa mwaka 2016)


        Na.

Aina

Mahitaji

Yaliyopo

%

Upungufu

%

1.

Vyumba vya madarasa

1,829

888

49

941

51

2.

Nyumba za walimu

1,829

334

19

1,495

81

3.

Vyoo (wavulana) matundu

2,144

6,886

32

1,458

68

4.

Vyoo (wasichana) matundu

2,144

684

32

1,460

68

5.

Ofisi za walimu wakuu

107

93

87

14

13

6.

Ofisi za walimu

121

80

66

41

34

7.

Madawati

29,446

19,647

67

9,799

33

8.

Viti

3,341

1,691

51

1,650

49

9.

Meza

3,034

1,326

44

1,708

56

10.

Matenki ya maji

134

69

51

65

49


    VITABU.

    Hadi Mwezi  Februari, 2016 uwiano wa kitabu kwa wanafunzi umefikia 1:5. Hii  ni baada ya kuanza kupokea vitabu  vilivyonunuliwa na Serikali (Capitation) na Shirika lisilo la kiserikali la  TWAWEZA na vitabu vya chenji ya Rada na wadau wengine.

VYUO VYA UFUNDI.
    Wilaya ina  Vyuo vya Ufundi 3 hadi kufikia mwaka huu 2016.   Chuo kimoja ni cha Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe (KDVTC), Chuo 1 ni  cha mtu binafsi (KVTC) na Chuo 1 ni cha Kanisa la Kilutheri Tanzania (Lukajange  ELCT).Vyuo hivi vinatoa elimu ya kuwawezesha vijana waweze kujitegemea na kujiajiri  katika fani mbali mbali.

ELIMU YA SEKONDARI
    IDADI YA SHULE KATIKA WILAYA 
    Wilaya ina jumla ya shule za Sekondari 25 zenye jumla ya wanafunzi 9,064 kati yao 4,330 wakiwa ni wavulana na 4,734 wasichana. Jedwali lifuatalo linaonesha idadi ya shule na wanafunzi         waliosajiliwa katika shule hizo.

Jedwali Namba 4: Idadi ya Shule za Sekondari kwa  mwaka 2015


        SHULE ZA SEKONDARI
SHULE
IDADI YA SHULE

WAVULANA

WASICHANA

JUMLA

Za Serikali

19

3,287

3,550

6,837

Zisizo za Serikali

6

1,043

1,184

2,227

JUMLA KUU

25

4,330

4,734

9,064


    IDADI YA WALIMU

    Kwa mwaka 2015 Wilaya  ina jumla ya walimu katika shule za sekondari za serikali 368. Kati yao 266 ni  wanaume na 102 ni wanawake.  

MIUNDO MBINU MUHIMU KATIKA SHULE 
    Hali ya uwepo wa miundombinu muhimu  katika Shule za Sekondari za Serikali ni kama inavyooneshwa katika jedwali  lifuatalo:-

Jedwali  Namba 5: Hali ya uwepo wa Miundombinu muhimu katika Shule za Serikali – 2015


        NA
AINA YA JENGO
MAHITAJI
YALIYOPO
%
UPUNGUFU
%

1

Madarasa

200

175

87

25

13

2

Nyumba za Walimu

368

41

11

260

89

3

Vyoo vya Walimu (ME)

38

19

50

19

50

Vyoo vya Walimu (KE)

38

19

50

19

50

4

Vyoo vya wanafunzi (ME) matundu

130

97

75

33

25

Vyoo vya wanafunzi (kE) matundu

177

112

63

65

37

5

Majengo ya utawala

19

7

37

12

63

6

Maktaba

19

0

0

19

100

7

Bwalo

19

1

5

18

95

8

Hosteli za wavulana

38

1

3

37

97

Hosteli  za    Wasichana

38

34

89

4

11

9

Vyumba vya Maabara

57

57

100

0

0

10
Majiko

19

1

5

18

95

 

UWEPO WA VITABU SHULENI
    Kimsingi, uwepo wa  vitabu vya kiada katika shule za sekondari za serikali kwa masomo yote tisa ya  msingi unaimarika mwaka hadi mwaka kwa namna serikali inavyoziwezesha shule  kununua vitabu kupitia fedha za ruzuku (capitation grant). Hadi mwezi Februari  2015 uwiano wa kitabu kwa wanafunzi upo kati ya wastani wa 1:3 na 1:1, hasa kwa  masomo ya sayansi na hisabati.

CHANGAMOTO
  
    Sekta ya Elimu ya Sekondari katika wilaya  inakabiliwa na changamoto za kimaendeleo kama ifuatavyo:-  

  •     
  • Upungufu  wa baadhi ya majengo muhimu katika shule hususani nyumba za walimu, hostel kwa  ajili ya wanafunzi, vyumba vya maktaba na majengo ya utawala ikiwa ni pamoja na  madawati.
  •     
  • Walimu  wanaokosa nyumba katika maeneo ya shule, wanalazimika kupanga katika nyumba za  mitaani au sehemu zisizo salama huko vijijini. Na wakati mwingine wanakosa  kabisa nyumba za kupanga.
  •     
  • Upungufu  wa walimu hasa wa masomo ya Sayansi na hisabati hupelekea shule kuajiri vijana  waliohitimu Kidato cha sita katika tahasusi za sayansi. Hawa hawana taaluma na  haiba ya ualimu.
  •     
  • Ukosefu  wa watumishi wa kuajiriwa wa kada za uhasibu, ukarani, Uboharia, Ulinzi, Upishi  na Uchapaji ni tatizo ambalo huwafanya walimu kufanya kazi ambazo siyo taaluma  yao, au shule kuajiri watumishi wa muda hivyo kuziongezea shule mzigo katika  bajeti zao.
  •     
  • Baadhi  ya shule zinakosa viwanja vya michezo kulingana na mazingira zilipo, lakini pia  na ufinyu wa eneo la shule husika.

MIKAKATI YA KUBORESHA TAALUMA KATIKA SHULE ZA  SEKONDARI    

  • Kuelimisha  jamii itambue kuwa jukumu la kukamilisha miundombinu muhimu shuleni ni la kila  mwananchi wa eneo husika.   
  • Kuhamasisha  wanajamii na wadau kutoa michango ya hali na mali itakayotosha kukamilisha  ujenzi wa miundombinu inayokosekana pamoja na uendeshaji wa shule kwa ujumla.   
  • Kuhamasisha  jamii kuziwezesha shule kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wote.    
  • Kushirikiana  na idara ya Ukaguzi wa Shule Wilaya na Kanda kuzikagua shule mara kwa mara ili  kushauri namna ya kuondoa mapungufu yaliyobainika na kuhakikisha kuwa usimamizi  na utoaji wa taaluma kwa wanafunzi wote unakuwa imara.    
  • Kuhamasisha  wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi na hisabati kwa bidii na nia ya dhati ili  hatimaye tuweze kupata Walimu wengi wa masomo ya Sayansi.    
  • Ili  kukabiliana na tatizo la upungufu wa shule za kidato cha tano na sita, wilaya  imeweka katika mpango wa maendeleo ya elimu ya Sekondari mkakati wa kukigeuza  chuo cha ualimu kilichokuwa kinajengwa kuwa shule ya sekondari ya A – level tu.  Lakini pia shule za sekondari Kituntu na Nyabiyonza zitaimarishwa kimiundombinu  kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha tano. 

CHUO CHA KILIMO CHA KARAGWE.
    Wilaya na wadau  wengine wa maendeleo, katika kuboresha sekta ya kilimo ambayo ndiyo uti wa  mgongo wa wananchi wa Karagwe inashirikiana na dhehebu la Dini la Kilutheri  Tanzania kupitia Dayosisi yake ya Karagwe       lilianza  ujenzi wa   chuo hicho. Lengo likiwa ni  kuwapata wataalamu wa kutosha wa kilimo watakaoweza kuongeza msukumo  katikakuinua sekta ya kilimo Wilayani na nchi nzima kwa ujumla. Aidha chuo hiki  kikikamilika kitakuwa chuo kikuu kikubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na  Kati.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 19, 2025
  • TANGAZO KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA KARAGWE September 02, 2025
  • TANGAZO LA KITWA KWENYE USAILI WA MAHOJIANO September 17, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMI 10 October 04, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MADIWANI 32 KARAGWE DC WAIANZA SAFARI YA UTUMISHI KWA WANANCHI (2025 - 2030) RASMI LEO.

    December 02, 2025
  • DC LAIZER AONGOZA KIKAO CHA TATHIMINI YA MKATABA WA LISHE KWA NGAZI YA KATA KWA ROBO YA KWANZA JULAI-SEPTEMBA

    November 14, 2025
  • DED MSANGA AKAGUA NA KUTEMBELEA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO

    September 29, 2025
  • WATUMISHI KARAGWE DC WAMSHUKURU DED KWA KUWEZESHA MAFUNZO YA AFYA YA AKILI.

    September 19, 2025
  • Angalia zote

Video

ZIARA YA WALIMU KATIKA HIFADHI YA TAIFA NGORONGORO
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • History
  • Dira na Dhamira
  • Fomu za mbalimbali
  • NEEMA INAKUJA KWA WAKULIMA
  • FEDHA ZILIZOPOKELEWA KWA AJILI YA MFUKO WA JIMBO

Viunganishi vihusishi

  • NECTA
  • UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAIFA
  • TAMISEMI
  • FFARS
  • SALARY SLIP

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    KARAGWE KAGERA TANZANIA

    Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE

    Simu: 028-2227148

    Simu ya mkononi: 028-2227148

    Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.