OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
--------------------------------------------------
HALMASHAURI YA WILAYA YA KARAGWE
Simu: 028-2227148 S. L. P. 20,
Fax: 028-2227140 KARAGWE
E-mail: innocent.mwalo@karagwedc.go.tz 24/05/2017.
TANGAZO KWA WATUMISHI WOTE NA UMMA KWA UJUMLA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hya Wilaya Karagwe, Godwin M. Kitonka anapenda kuwaomba watumishi na wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya kwa ujumla kuchangia mbio za mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani hapa mnamo Agosti, 04, 2017.
Ikiwa ni azimio lililofikiwa kwenye kikao cha kamati ya Mwenge wa Uhuru kilichoketi mapema mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu, kila Mkuu wa Idara katika Halmashauri hii anaombwa kuchangia kiasi cha Tsh. 30,000/= huku maafisa wengine wakiombwa kuchangia kiasi cha Tsh. 10,000/= kila mmoja.
Wakuu wa shule za Msingi na Sekondari pamoja na Waratibu Kata watapaswa kuchangia kiasi cha Tsh. 20,000/= kila mmoja.
Aidha, walimu wa shule za Sekondari, wahudumu na madereva wanaombwa kuchangia kiasi cha Tsh.5,000/= kila mmoja huku walimu wa shule za msingi wakitakiwa kuchangia kiasi cha Tsh. 3,000/= kila mmoja.
Hata hivyo, Afisa Biashara Wilaya anaagizwa kukusanya michango kwa baadhi ya vyombo vya moto ambapo kila teksi inaombwa kulipa kiasi cha Tsh.5,000/= na kwa upande wa mabasi kila moja likitakiwa kuchangishwa kiasi cha Tsh.50,000/=
Kwa upande wao wafanya biashara wadogo wanaombwa kuchangia kiasi cha Tsh. 10,000/= kila mmoja.
Shule na Taasisi binafsi na wazabuni wote wanaombwa mchango wa kiasi cha Tsh. 50,000/= kila mmoja, huku shule za msingi na sekondari za serikali zikiombwa kiasi cha Tsh.20,000/=
Ikimbukwe kuwa kila Mkuu wa Idara na yeyote alipewa jukumu hilo la ukusanyaji atapaswa kutoa taarifa ya ukusanyaji katika kila kikao cha kamati ya mwenge kitakapokaa.
Inashauriwa kuwaelimsha wachangiaji kuona umuhimu wa kuchangia mchango huu kwani kwa mchango huu ni wa hiari.
Imetolewa na
Innocent E. Mwalo,
Afisa Habari,
Halashauri ya Wilaya,
Karagwe
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.